Updated Thursday, April 13, 2017

Watu zaidi ya 600,000 waondolewa mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang


Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini amewaamuru asilimia 25% ya raia wake kutoka mji mkuu wa Pyongyang kuondoka mara moja. 

Inakadiliwa watu zaidi ya 600,000 wataondoka katika mji huo, hii ni kutokana na hadi ya tahadhali iliyopo kati ya Marekani na Korea.

Sehemu za kuwahifadhi watu ili wasithurike na mabomu ni chache ukilinganisha na wingi wa watu katika eneo hilo; watu wote waliokwisha patikana na makosa ya jinai wanatakiwa waondoke katika mji huo ili kuwapa nafasi wengine kuwa na hifadhi nzuri ya kujikinga dhidi ya mabomu.

Pia inasemekana kuna manuari ya kubeba maroketi ipo njiani kuelekea peninsula ya Korea ili kuungana na vikosi vya Marekani vilivyopo eneo hilo.

Pia Japan imesema itatoa raia wake wote waliopo Korea ya Kusini kutokana na hali ya hatari kuongezeka katika ukanda huo.

Watu zaidi ya 600,000 waondolewa mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang Watu zaidi ya 600,000 waondolewa mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang Reviewed by Bill Bright Williams on 8:11:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.