Updated Thursday, April 6, 2017

Syria yasema kemikali za sumu zinatoka kwa magaidi waliopo Uturuki


Syria imezidi kuonya baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba magaidi toka Uturuki na Iraq ndio wanaingiza kemikali za sumu nchini mwao.

Waziri wa mambo ya nje nchini Syria Walid Muallem alisema siku ya alhamisi kwamba al-Nusra Front wanahusika kwa karibu zaidi kwenye shambulio la sumu lililoua watu 80.

"al-Nusra Front,ISIL na vikundi vingine vya kigaidi wanazidi kuleta kemikali za sumu na kuzihifadhi kwenye miji na makazi ya watu. Na tumeshatoa taarifa sana kwenye baraza la usalama na vyombo vingine vinavyohusika na kemikali za sumu, kuwapa maelezo kuhusu kemikali zinazoingizwa nchini Syria zikitokea Iraq na Uturuki," Muallem  alisema.

Syria yasema kemikali za sumu zinatoka kwa magaidi waliopo Uturuki Syria yasema kemikali za sumu zinatoka kwa magaidi waliopo Uturuki Reviewed by Bill Bright Williams on 10:33:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.