Updated Thursday, April 13, 2017

Msifananishe Korea Kaskazini na Syria, Beijing imeionya Marekani


China imeionya Marekani dhidi ya kutaka kutumia jeshi kuipiga Korea Kaskazini, Baada ya kuenea manuari za kivita katika rasi ya Korea.

Mvutano mkali umezidi zaidi mara baada ya raisi wa Marekani, Donald Trump kusema atakabiliana na matatizo ya Korea Kaskazini bila ya kuishirikisha China. Onyo hili limekuja mara baada ya manuari za kubeba ndege 'USS Carl' kukaribia mpaka wa Korea na wiki moja tu mara baada ya Trump kuruhusu kushambuliwa kwa makombora katika kikosi cha anga cha Syria.

China imeonya kutumia nguvu dhidi ya Pyongyang.

"Kutumia nguvu za kijeshi hakuwezi kutatua tatizo," Amesema waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi.

Na pia gazeti maarufu la Global Times katika habari zake limeandika,'Pyongyang ina uwezo wa kukabiliana na Korea kusini, Japo kuwa Pyongyang ina uwezo na nguvu za kinyuklia, kama dirty bomb wakiamua kulirusha Korea Kusini italeta mchafuko wa kinyuklia, kitu ambacho ni kigumu kuvumilika kwa wa Korea Kusini ambao ni vibaraka wa Marekani'

Msifananishe Korea Kaskazini na Syria, Beijing imeionya Marekani Msifananishe Korea Kaskazini na Syria, Beijing imeionya Marekani Reviewed by Bill Bright Williams on 3:31:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.