Updated Thursday, April 6, 2017

Msichana agunduliwa kuishi na nyani msituni India


Msichana mmoja amegunduliwa kuishi kwa muda usiojulikana na nyani porini nchini India .
Mamlaka nchini India imegundua msichana aliyekuwa anaishi na nyani porini na hivi sasa wanajaribu kutafuta utambulisho wa msichana huyo.

Msichana huyo anaaminika kuwa na miaka 10 au 12.

Msichana huyo alikuwa hana uwezo wa kuongea,hana nguo na alionekana mwenye udhaifu wa mwili.

Mtoto huyo wa kike alikuwa na tabia kama ya mnyama wa porini akiruka ruka kwa kutumia  mkono yake pamoja na miguu huku akichukua chakula kutoka sakafuni akitumia mdomo wake .

Baada ya matibabu alianza kuwa kama mwanadamu wa kawaida na kula kwa kutumia mikono yake .

Madaktari wameripoti kuwa bado hana uwezo wa kuongea ila amaeanza kuelewa anachoambiwa na hata kutabasamu .

Mnamo mwezi Januari walinzi porini waligundua msichana mmoja aliyekuwa anazunguka zunguka na nyani kadhaa nchini India .

Baadaye maafisa wa polisi walienda kumchukua ambapo nyani hao waliwavamia .

Polisi wanaendelea kufanya uchunguzi wa utambulisho wake na kutafuta wazazi wake.

Msichana agunduliwa kuishi na nyani msituni India Msichana agunduliwa kuishi na nyani msituni India Reviewed by Bill Bright Williams on 11:16:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.