Updated Sunday, April 9, 2017

Miripoko ya kigaidi yatokea katika makanisa nchini MisriRais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi atangaza miezi mitatu ya hali ya dharura baada ya mashambulizi mawili ya bomu  kutekelezwa katika makanisa mawili nchini Misri.

Mripuko wa kwanza umetokea katika kanisa la kabila la Kibti liliopo katika mji wa Tanta kaskazini mwa mji mkuu wa Misri Cairo ambapo ulipelekea kuuwawa watu 20 na wengine 30 kujeruhiwa nchini humo.

Jeshi la Polisi nchini humo linasema kuwa mripoko mwingine pia ulitokea katika Kanisa moja la Wakibti katika mji wa Alexandria katika fukwe za bahari ya Mediterranean.

Wizara ya afya nchini Misri imesema kuwa kufuatia mripuko wa kwanza uliotokea katika sehemu ya Tanta, ambapo mpaka sasa watu 20 wamepoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa, ambapo viongozi wa wizara ya afya wanasema kuwa idadi ya watu waliouwawa yawezekana ikazidi.

Mji wa Tanta uko pembeni mwa mto Nile, ambapo iko umbali wa kilometa 120 kwenda kaskazini mwa mji wa Cairo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Televisheni ya taifa la nchi hiyo, zimetangaza kutokea kwa mripuko mwingine katika mji wa Alexandria ambapo mtu mmoja alikuwa amevaa bomu alikuwa akifanya juhudi za kutaka kuingia katika Kanisa la mtakatifu Marko na polisi walifanikiwa kumzuia gaidi huyo kuingia ndani ya Kanisa hilo, ndipo gaidi huyo akaamua kujiripua hatimaye Polisi naye kuuwawa pamoja na gaidi huyo.

Mripuko huo umetokea katika hali ambayo Wakristo wa Misri walikuwa wakifanya sherehe za sikukuu ya Sabasib, ambayo ni katika sherehe na sikuku za Wakristo hao.

Kikundi cha kigaidi cha Daesh kimetangaza kuhusika na tukio hilo la kigaidi dhidi ya wakazi wachache wa Kibti wanaoishi nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.  
Miripoko ya kigaidi yatokea katika makanisa nchini Misri Miripoko ya kigaidi yatokea katika makanisa nchini Misri Reviewed by Bill Bright Williams on 11:47:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.