Updated Thursday, April 6, 2017

Marekani yaonya uwezo wa Korea Kaskazini kutengeneza makombora yenye vichwa vya nyuklia


Afisa wa juu wa jeshi la Marekani ametoa onyo kuwa ni kitambo kidogo tu kabla ya Korea Kaskazini kurusha makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kuvuka mabara yenye vichwa vya nyuklia.

Mkuu wa kamandi ya kimkakati ya Marekani, Kamanda John Hyten, alitoa ushahidi juu ya mipango ya nyuklia na makombora ya Korea Kaskazini kwenye kikao cha kamati ya seneti siku ya Jumanne. Kamandi ya kimkakati inahusika na ulinzi unaohusisha makombora.

Hyten alisema kitendo cha Korea Kaskazini kurusha kombora la fueli mango la masafa ya kati mnamo mwezi Februari, kutoka kwenye mtambo unaohamishika wa kurushia makombora, kinaashiria teknolojia mpya. Aliita uwezo huo mpya wa Korea Kaskazini "Changamoto kali". Ofisa huyo ametoa onyo pia kuwa lolote litakalofanywa na Korea Kaskazini halitabiriki.
Marekani yaonya uwezo wa Korea Kaskazini kutengeneza makombora yenye vichwa vya nyuklia Marekani yaonya uwezo wa Korea Kaskazini kutengeneza makombora yenye vichwa vya nyuklia Reviewed by Bill Bright Williams on 4:18:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.