Updated Thursday, April 13, 2017

Marekani imeipiga Afghanistan kwa bomu kubwa sana, hii ni mara ya kwanza kwa bomu hili kutumika vitani


Jeshi la Marekani kwa mara ya kwanza limetumia bomu aina ya GBU-43/B Massive Ordnance Air Blast Bomb (MOAB) maarufu kama mama wa mabomu yote ulimwenguni nchini Afghanistan kwa ajili ya kuharibu njia zote za wapiganaji wa kiislamu nchini humo.

Bomu hilo lina kilo 9525kg, limeangushwa katika wilaya ya Achin katika jimbo la Nangarhar mashariki ya Afghanistan. 
Pentagon imethibitisha matumizi ya bomu hilo, na hadi sasa haijafahamika ni watu wangapi wameangamia kwa silaha hiyo hatari.

Bomu hili lilitengenezwa mnamo mwaka 2003, na alikuwahi kutumika popote pale toka mwaka huo hadi leo alhamisi mida ya saa moja usiku.
Bomu hili liliundwa kwa ajili ya kuharibu maeneo makubwa chini ya ardhi, mlipuko wake ni kama bomu la nyuklia,'Luteni Rick Francona ameiambia CNN.

Marekani imeipiga Afghanistan kwa bomu kubwa sana, hii ni mara ya kwanza kwa bomu hili kutumika vitani Marekani imeipiga Afghanistan kwa bomu kubwa sana, hii ni mara ya kwanza kwa bomu hili  kutumika vitani Reviewed by Bill Bright Williams on 10:53:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.