Updated Tuesday, April 4, 2017

Kemikali ya sumu inayoathiri mishipa ya fahamu yahofiwa kuua 67 Syria


Shirika moja lisilo la kiserikali linalofanya kazi katika maeneo yaliyokumbwa na mapigano ya vita nchini Syria limesema kemikali hatari ya sumu inayofanana na sarin inayoathiri mishipa ya fahamu huenda imetumika katika shambulio la anga lililoua watu 67 jana Jumanne.

Watu wengi katika jimbo la Idlib lililopo Kaskazini magharibi mwa Syria wamepatwa na dalili zinazofanana na shambulio la kemikali baada ya shambulio la anga la juzi Jumanne. Dalili hizo ni pamoja na matatizo ya kupumua, kutapika na kutetemeka. 

Shirika hilo lisilo la kiserikali ambalo limekuwa likisaidia taasisi za tiba nchini Syria limesema shambulio hilo limeua watu 67 wakiwemo watoto na kujeruhi wengine takribani 200 ambao wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini.

Wafanyakazi wa misaada katika shirika hilo wamesema kuwa baadhi ya waathirika wa shambulio hilo wamesinyaa mboni za macho. Wamesema hiyo imewafanya kuamini kuwa kemikali ya sarin au zingine zinaathiri mishipa ya fahamu ilitumika. 

Hata hivyo serikali ya Syria chini ya Rais Bashar al-Assad kupitia taarifa iliyotolewa na chombo cha habari cha serikali imepinga madai ya vikosi vya waasi kuwa serikali ilitumia sihala za kemikali. Badala yake serikali imeshutumu kuwa waasi ndiyo waliotekeleza shambaulio hilo.
Kemikali ya sumu inayoathiri mishipa ya fahamu yahofiwa kuua 67 Syria Kemikali ya sumu inayoathiri mishipa ya fahamu yahofiwa kuua 67 Syria Reviewed by Bill Bright Williams on 10:36:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.