Updated Thursday, April 20, 2017

ISIS wadai kuhusika na shambulio la kigaidi jijini Paris UfaransaPolisi wawili wauawa katika shambulizi la silaha linalodaiwa kutekelezwa na ISIS.
Mshambuliaji mmoja ameripotiwa kushambulia polisi kwa risasi siku ya Alhamis majira ya jioni eneo la Champs Elysees mjini Paris .

Polisi wawili wameripotiwa kuuawa huku afisa mmoja kujeruhiwa vibaya wakati huo wa shambulizi hilo.

Baada ya tukio hilo kundi la Daesh lilitangaza kuhusika na shambulio hilo.

Msemaji wa polisi Johanna Primevert alifahamisha kuwa magaidi hao walikuwa wanalenga maafisa wa usalama waliokuwa wanalinda eneo karibu na kituo cha Franklın Roosevelt ambapo kawaida huwa na idadi kubwa ya watalii.

Baada ya tukio polisi walifunga barabara zote za eneo hilo na kutaka watalii wote kurudi katika hoteli kwa usalama wao.

Shambulizi hilo limetokea siku tatu kabla ya duru ya kwanza ya kura katika uchaguzi wa rais nchini Ufaransa .

Tangu siku ya Jumanne kumekuwa na ulinzi mkali baada ya polisi kufahamisha kuwa kuna uwezekano wa kutekelezwa shambulizi la kigaidi na kukamatwa kwa washukiwa wawili.
ISIS wadai kuhusika na shambulio la kigaidi jijini Paris Ufaransa ISIS wadai kuhusika na shambulio la kigaidi jijini Paris Ufaransa Reviewed by Bill Bright Williams on 9:54:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.