Updated Monday, April 10, 2017

China yatuma wanajeshi 150,000 katika mpaka wa Korea Kaskazini


Kitu kilichoshitua sana wiki iliopita ni kile kitendo cha jeshi la Marekani, kurusha makombora dhidi ya vikosi vya Bashar al Assad nchini Syria. Trump alitoa ujumbe kutoridhishwa na shambulio la gesi lililoua watu 70, wengi wao wakiwa watoto, na sasa lengo lake linahamia Korea Kaskazini.

Marekani wameisogeza karibu manuari ya kinyuklia Calvinus(CVN-70) hadi Singapore, na China nayo imelisogeza karibu zaidi kundi lake la wanajeshi 150,000 mpakani mwa Korea Kaskazini kwa maandalizi ya shambulio lolote litakaloweza kujitokeza.


Kwa mujibu wa chosun, moja kati ya mawakala wakubwa wa habari nchini Korea Kusini,ameshuhudia vikosi vya China, na anasema China wameshitushwa sana na kitendo cha Marekani kuishambulia Syria, na vikosi vilivyotumwa mpakani ni kwa ajili ya kujibu shambulio lolote litakalotokea.

China yatuma wanajeshi 150,000 katika mpaka wa Korea Kaskazini China yatuma wanajeshi 150,000 katika mpaka wa Korea Kaskazini Reviewed by Bill Bright Williams on 11:40:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.