Updated Monday, March 27, 2017

UN yaanza majadiliano ya kupiga marufuku silaha za nyuklia


Mkutano wa majadiliano kuhusu mkataba wa kisheria wa kupiga marufuku silaha za nyuklia unaanza leo Jumatatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York nchini Marekani. Hata hivyo nchi zote zenye silaha za nyuklia hazitashiriki.

Mkutano mkuu wa umoja wa Mataifa uliofanyika Desemba mwaka jana ulipiga kura kuwa majadiliano ya suala hilo yaanze. Nchi zaidi ya 50 zisizo na silaha za nyuklia ziliwasilisha mapendekezo yao na nchi 113 kati ya hizo ziliunga mkono azimio hilo. 

Mkataba huo una lengo la kupiga marufuku silaha za nyuklia kwa tafsiri kwamba zinakiuka sheria za kimataifa. Mataifa zaidi ya 100 yanatarajiwa kushiriki majadiliano hayo. Watajielekeza kuhusu namna ya kuzuia kisheria matumizi ya silaha za nyuklia. 

Marekiani na Urusi zinasema kuwa majadiliano hayo hayana msingi wa kwa mtazamo wa usalama wa kimataifa. Japani ambayo ni nchi pekee iliyowahi kupitia tajiriba ya kushambuliwa kwa mabomu ya atomiki nayo imeonekana kutounga mkono mkataba huo.

Msimamo wa serikali ya Japani ni kwamba mchakato wa kuachana na silaha za nyuklia unatakiwa kufanyika hatua kwa hatua kwa kushirikisha mataifa yenye silaha hizo na yale yasiyo nayo. Japani imepanga kumtuma mjumbe wake kuzungumza katika mkutano huo lakini haiko tayari kushiriki majadiliano hayo. 

Alhamisi iliyopita, Waziri wa mambo ya Nje wa Sweden, Margot Wallstrom alisema katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuwa majadiliano hayo yanafanyika kwa wakati mwafaka. Alisema kumekuwa na maoni ya hivi karibuni yanayoonesha kujivunia silaha za nyuklia. 

Waziri huyo wa Sweden aliongeza kusema kwamba nchi nyingi zinapata wasiwasi kuhusu kukwama kwa juhudi za kuachana na matumizi ya silaha za nyuklia.
UN yaanza majadiliano ya kupiga marufuku silaha za nyuklia UN yaanza majadiliano ya kupiga marufuku silaha za nyuklia Reviewed by Bill Bright Williams on 3:34:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.