Updated Tuesday, March 14, 2017

Russia kuteketeza silaha zote za kemikali nchini humo mwaka huu


Mwenyekiti wa Kamati ya Kupunguza Silaha za Kemikali ya Russia Mikhail Babich amesema nchi hiyo inaweza kuteketeza silaha zake zote za aina hiyo mwaka huu.

Akiwa kwenye mkutano na rais Vladmir Putin wa Russia, Babich amesema nchi hiyo iko katika hatua ya mwisho ya kutekeleza Mkataba wa Kudhibiti Silaha za Kemikali, uliosainiwa na nchi 192 na kuanza kutekelezwa mwaka 1997. Pia amesema, Russia imetumia dola za Kimarekani bilioni 5.6 kwa ajili ya kuharibu silaha za kemikali, na tayari imeanzisha shule na hospitali katika eneo la vifaa vyenye silaha hizo ili kusaidia wahusika kupata ajira.
Russia kuteketeza silaha zote za kemikali nchini humo mwaka huu Russia kuteketeza silaha zote za kemikali nchini humo mwaka huu Reviewed by Bill Bright Williams on 9:43:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.