Updated Monday, March 27, 2017

Rapper Nay wa Mitego aachiwa huru kwa agizo la Rais


Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania  Emmanuel Elibariki, akijulikana kwa jina la Nay wa Mitego, ameachiwa huru siku moja baada ya kushikwa kwa kutoa wimbo uliokuwa unaonekana kuikosoa serikali.

Wimbo huo ulikuwa umefungiwa na BASATA, Agizo la kuachiwa kwa Ney wa Mitego lilitolewa na waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma.

Dkt Mwakyembe alisema kuwa rais Magufuli amesema wimbo huo ni mzuri na kumshauri Nay wa Mitego aimbe mambo mengine kama kuwataja watu ambao wanakwepa kulipa kodi na watumiaji wa dawa za kulevya.

Rapper Nay wa Mitego aachiwa huru kwa agizo la Rais Rapper Nay wa Mitego aachiwa huru kwa agizo la Rais Reviewed by Bill Bright Williams on 9:49:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.