Updated Tuesday, March 7, 2017

Rais wa Tanzania aagiza Tanesco kuwakatia umeme wenye madeni suguRais wa Tanzania John Magufuli jana aliiagiza kampuni ya ugavi wa umeme nchini humo (Tanesco) kuwakatia umeme wateja wote wenye madeni makubwa kwa kampuni hiyo, ikiwemo serikali ya Zanzibar, limeripoti gazeti la The Citizen.

Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo kipya cha Tanesco mkoani Mtwara, rais Magufuli alisema kuwa tasisi zote za umma zinapaswa kulipa madeni la sivyo zitakatiwa umeme.

Alisema kuwa serikali ya Zanzibar pekee , kupitia shirika la umeme za Zanzibar (Zeco), ina deni la Tanesco kiasi cha shilingi bilioni 121 za Tanzania.
Rais wa Tanzania aagiza Tanesco kuwakatia umeme wenye madeni sugu Rais wa Tanzania aagiza Tanesco kuwakatia umeme wenye madeni sugu Reviewed by Bill Bright Williams on 2:47:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.