Updated Wednesday, March 22, 2017

Rais Uturuki hatakiwi tena Ujerumani


Mshirika wa ngazi ya juu wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan amevuka mpaka kwa kuilinganisha serikali ya Ujerumani na utawala wa kidikteta wa Hitler .  

Volker Bouffier, naibu mwenyekiti wa chama cha Christian Democratic Union CDU cha kansela Merkel amesema rais Erdogan hakaribishwi tena Ujerumani. Kauli ya Bouffier inadhihirisha kuongezeka kwa hali ya kutoridhisha iliyosababishwa na kauli za Erdogan kwamba Ujerumani na mataifa mengine ya Ulaya yanatumia mbinu za manazi kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya Uturuki.

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeripoti kwamba Erdogan anapanga kuitembelea Ujerumani mwezi huu kuwashawishi wapiga kura takriban milioni 1.4 wa Uturuki wanaoishi humu nchini kuunga mkono mabadiliko ya katiba yatakayompa madaraka mapya rais katika kura ya maoni iliyopangwa kufanyika Aprili 16.
Rais Uturuki hatakiwi tena Ujerumani Rais Uturuki hatakiwi tena Ujerumani Reviewed by Bill Bright Williams on 12:47:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.