Updated Saturday, March 11, 2017

Raia wapatao 70 wa Somalia wafukuzwa Marekani


Raia wapatao 70 wa Somalia waliofukuzwa  Marekani wamefika Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.

Waziri wa usalama wa nchini wa Somalia amesema hii ni mara ya pili kwa Marekani kurejesha raia wa Somalia mwaka huu. Wasomali hao wameishi katika kituo cha kizuini nchini Marekani kwa miaka miwili, lakini hawajapata hadhi halali ya kuishi nchini humo.

Kabla ya hapo raia wapatao 90 wa Somalia walirejeshwa na Marekani mwishoni mwa mwezi Januari.

Tarehe 21 Februari wizara ya usalama wa ardhi ya Marekani ilitoa nyaraka mbili ambazo si kama tu zimeongeza orodha ya wahamiaji haramu wanaotakiwa kufukuzwa, bali pia zimepanga kuharakisha kazi ya kuwafukuza wahamiaji hao.
Raia wapatao 70 wa Somalia wafukuzwa Marekani Raia wapatao 70 wa Somalia wafukuzwa Marekani Reviewed by Bill Bright Williams on 11:24:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.