Updated Friday, March 31, 2017

Njia 5 za kuweka figo zako katika afya bora


Siku ya figo duniani ni siku ya kimataifa ikiwa na lengo la kukuza ufahamu kuhusu umuhimu wa figo. Figo ziko na umbo kama maharage yenye ukubwa wa ngumi. Kila siku figo zinachuja lita 120 hadi 150 za damu na kuzalisha lita 1 hadi 2 za mkojo, ikijumuisha maji taka na taka za ziada.
Kwa mujibu wa taasisi ya Kisukari na Magonjwa ya figo, figo ni ugonjwa unaoua kimyakimya.

Hizi ni njia za kuweka figo zako katika afya bora;

1.Kunywa maji mengi
Mwili usiokuwa na maji mengi, unakuwa hauna uwezo wa kutoa sumu na uchafu kwenye mfumo wake."Wakati maji mwilini yakipungua, kutatokea upungufu wa damu toka tumboni na kwenye figo, kwa hiyo wingi wa damu utapendelea kwenda kwenye moyo na ubongo.Na pia Dr Joseph N. Chorley kutoka Hospitali ya Texas ya Watoto, anasema,"kupungua damu kwenye figo, kutasababisha upungufu wa virutubisho na oksijeni kwenye figo na matokeo yake figo uharibika"  

2.Acha kuvuta sigara
Sigara ufufua shinikizo la damu.Pia uharibu baadhi ya madawa yanayotumika kutibu shinikizo la damu. Uvutaji wa sigara upunguza mtiririko wa damu kwenye viungo muhimu, ikiwa ni pamoja na figo.Inafanya mishipa ya damu kenye figo kusinyaa.

3.Fanya mazoezi mara kwa mara
Mazoezi yana uwezo wa kukuepusha na uzito mkubwa na hata shinikizo la damu.Utafiti unaonyesha mazoezi mazuri kwa figo yako ni pamoja na kutembea,kuogelea, kuendesha baiskeli, na kucheza.

4.Weka kiwango cha sukari katika damu kwenye uwiano mzuri
Kiwango kikubwa cha sukari katika damu kitafanya figo kufanya kazi ngumu na kuchuja damu nyingi mno, kwa figo kufanyakazi ngumu ya kuchuja, itasababisha uchafu kubaki kwenye damu, ambapo matokeo yake figo itashindwa kufanya kazi. Pia wingi wa sukari kwenye damu husababisha shinikizo la damu.

5.Shinikizo la damu
Shinikizo la damu husababisha magonjwa ya figo,na pia utafiti unaonyesha kuwa wavutaji sigara enye kisukari au shinikizo la juu la damu wapo kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa ya figo.Njia 5 za kuweka figo zako katika afya bora Njia 5 za kuweka figo zako katika afya bora Reviewed by Bill Bright Williams on 5:10:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.