Updated Friday, March 31, 2017

Mwili wa Kim waondoka kuelekea Korea Kaskazini


Wanaume wawili wanaoaminika kuwa raia wa Korea Kaskazini waliokuwa wakisakwa na polisi wa Malaysia ili kuhojiwa, wameondoka kuelekea nchini kwao baada ya kusimama kwa muda jijini Beijing nchini China.

Wanaume hao wanashukiwa kuhusika kwenye shambulio la mauaji ya Kim Jong Nam ambaye ni kaka wa kambo wa Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini mwezi Februari mwaka huu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China iliwaambia waandishi wa habari jana Ijumaa kuwa ndege iliyokuwa imewabeba watu hao na mwili wa marehemu iliondoka kuelekea Korea Kaskazini.

Mmoja wa wanaume hao anaaminika kuwa ni Hyon Kwang Song, ambaye ni afisa msaidizi wa pili wa ofisi za kibalozi za Korea Kaskazini jijini Kuala Lumpur, Malaysia. Mwingine anadhaniwa kuwa ni Kim UK II, mwajiriwa wa shirika la ndege linalomilikiwa na Korea Kaskazini.

Uhusiano kati ya Malaysia na Korea Kaskazini ulizorota katika siku za hivi karibuni. Nchi hizo mbili zilichukua hatua zisizo za kawaida kuwazuia kuondoka raia wa kigeni wa nchi hizo.

Hata hivyo serikali ya Malaysia ilisema juzi Alhamisi usiku kuwa itawaruhusu raia wote wa Korea Kaskazini kuondoka nchini humo. Korea Kaskazini pia ilitoa taarifa kama hiyo.

Wachunguzi wanasema Korea Kaskazini huenda ikayapa nguvu madai yake kuwa haikuhusika kwenye mauaji ya Kim kutokana na hatua ya kukabidhiwa mwili huo wa marehemu.

Mwili wa Kim waondoka kuelekea Korea Kaskazini Mwili wa Kim waondoka kuelekea Korea Kaskazini Reviewed by Bill Bright Williams on 11:34:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.