Updated Thursday, March 30, 2017

Mtoto wa Trump kuwa mshauri wa baba yake White House


Taarifa kutoka ikulu ya Marekani ya White House zimefahamisha kuwa Ivanka Trump mtoto wa kike wa rais Donald Trump atahudumu kama mshauri wa rais ikulu.

Katika ajira hiyo, Ivanka Trump hatopokea mshahara kwa jukumu alilolichukuwa na kuwa mshauri wa baba yake.

Ivanka Trump atakuwa kama mfanyakazi wa kujitolea katika ofisi ya baba yake ikulu White House.

Ivanka Trump alifahamisha kuwa baada ya  kufikiria kuhusu kazi hiyo  ameamua kuwa mshauri wa baba yake bila ya malipo akihofia tuhuma za upendeleo.

Ivanka ana umri wa miaka 35.

Ivanka kumshauri baba yake kumezua ukosoaji dhidi ya rais Trump na kunyooshewa kidole cha lawama  na tuhuma za upendeleo wa kifamilia.

Vile vile  kunahofiwa kuwa na uvujaji wa siri za serikali.
Mtoto wa Trump kuwa mshauri wa baba yake White House Mtoto wa Trump kuwa  mshauri wa baba yake White House Reviewed by Bill Bright Williams on 4:53:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.