Updated Monday, March 27, 2017

Msanii wa Rap nchini Tanzania ameshikwa na polisi kwa kumkosoa rais


Mwanamuziki maarufu nchini Tanzania Emmanuel Elibariki a.k.a Nay wa Mitego, amekamatwa na polisi kwa kuuachia wimbo wake unaotuhumiwa kuikosoa serikali.

Wimbo huo kwa jina la "WAPO" ulianza kusikika wiki iliopita na umeanza kupata sana umaarufu kwa watu ku-share kwenye mitandao ya kijamii.

Nay wa Mitego amekamatwa siku chache baada ya rais John Magufuli kuonya vyombo vya habari kuwa makini kwa uhuru walionao sasa.

Polisi wamethibitisha kukamatwa kwa mwanamuziki huyo na wamesema watamuhoji kwa maneno aliyoongea kwenye mwimbo huo.
Moja ya mashairi ya wimbo huo yanasema,"hakuna uhuru wa habari wala taarifaya habari, wanapindisha pindisha kuiogopa serikali"
Msanii wa Rap nchini Tanzania ameshikwa na polisi kwa kumkosoa rais Msanii wa Rap nchini Tanzania ameshikwa na polisi kwa kumkosoa rais Reviewed by Bill Bright Williams on 4:18:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.