Updated Wednesday, March 22, 2017

Marekani yazuia abiria kuingia na vifaa vya kielekitroniki kwenye ndege


Wizara ya usalama wa ndani ya Marekani imetangaza kuwazuia abiria wanaosafiri moja kwa moja na ndege kutoka viwanja kumi vya ndege katika nchi nane za Mashariki ya Kati na Afrika kwenda Marekani, kuingia na vifaa vya kielekitroniki kwenye mizigo yao ya mikononi.

Taarifa inasema tathimini ya kiusalama inaonyesha kuwa katika miaka ya hivi karibu ndege za abiria zimekuwa ni shabaha ya shambulizi la kigaidi , na makundi ya kigaidi yanapanga mbinu mpya za shambulizi zikiwemo kuweka vilipuzi katika vifaa mbalimbali za kielekitroniki.

Viwanja hivyo 10 viko Jordan, Uturuki, Saudi Arabia, Kuwait, Misri, Qatar, Falme za kiarabu na Morocco. Vifaa vya kielekitroniki vinaweza kusafirishwa kwenye mizigo iliyokaguliwa, na simu za mkononi na vifaa vya matibabu havijazuiliwa.

Baada ya Marekani kutoa tangazo hilo, Uingereza pia imetangaza zuio kama hilo kwa ndege kutoka Uturuki, Lebanon, Misri, Saudi Arabia, Jordan na Tunisia.
Marekani yazuia abiria kuingia na vifaa vya kielekitroniki kwenye ndege Marekani yazuia abiria  kuingia na vifaa vya kielekitroniki kwenye ndege Reviewed by Bill Bright Williams on 9:04:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.