Updated Monday, March 27, 2017

Maandamo makubwa ya upinzani yafanyika Urusi


Maelfu ya watu jana Jumapili walijitokeza katika maandamano yaliyofanyika kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Moscow na miji mingine nchini Urusi. Maandamano hayo yalikuwa na lengo la kumpinga Rais Vladimir Putin na kile wanachotafsiri kama rushwa ya kisiasa. 

Maandamano hayo ya jana Jumapili yalifanyika ili kuunga mkono wito wa kuchukua hatua uliotolewa na kiongozi wa upinzani Alexei Navalny. Polisi nchini humo wanasema zaidi ya watu 10,000 walishiriki kwenye maandamano hayo. 

Maandamano makubwa kuliko yote yalifanyika kwenye mji mkuu wa Moscow ambapo watu 8,000 walihudhuria. Maandamano hayo yalikuwa makubwa kuliko yote yaliyofanyika baada ya yale ya kumpinga Putin yaliyofanyika wakati wa uchaguzi mkuu wa uraisi wa mwaka 2012.

Kwa vile mamlaka hazikutoa ruhusa kwa maandamano hayo kufanyika, takribani watu 500 akiwemo Navalny walishikiliwa na polisi. Navalny ameongeza ukosoaji wake dhidi ya utawala wa Putin. Pia ametangaza nia yake ya kugombea urais kwenye uchaguzi ujao.

Rais Putin bado ananufaika na uungwaji mkono mkubwa, lakini wananchi wenye kipato cha kati wanaoishi mijini wanazidi kukasirishwa na hali ya kusuasua kwa uchumi.
Maandamo makubwa ya upinzani yafanyika Urusi Maandamo makubwa ya upinzani yafanyika Urusi Reviewed by Bill Bright Williams on 3:08:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.