Updated Tuesday, March 14, 2017

Kenya kujenga kituo cha umeme cha nyuklia kabla ya mwaka 2027


Kenya imesema inapanga kujenga kituo cha kwanza cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia kabla ya mwaka wa 2027. 

Waziri wa nishati na mafuta wa nchi hiyo Bw. Charles Keter amesema kabla ya kutimiza ndoto hiyo, Kenya inatakiwa kufikia vigezo vikali vilivyowekwa na Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA. 


Kwa mujibu wa waziri huyo, Kenya inapanga kutumia dola za kimarekani bilioni 5 kujenga kituo hicho, ambacho kinatarajiwa kuongeza maradufu uwezo wa kuzalisha umeme nchini humo.
Kenya kujenga kituo cha umeme cha nyuklia kabla ya mwaka 2027 Kenya kujenga kituo cha umeme cha nyuklia kabla ya mwaka 2027 Reviewed by Bill Bright Williams on 10:54:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.