Updated Thursday, March 30, 2017

Kamati ya Bunge la Marekani lapitisha hatua kali dhidi ya Korea Kaskazini


Kamati ya Bunge la Marekani limepitisha hatua kali dhidi ya Korea Kaskazini kutokana na vitendo vyake vya kuendelea kutengeneza makombora pamoja na vitendo vingine vya kichokozi.

Mapendekezo hayo yaliyopitishwa na kamati ya bunge ya masuala ya nje jana Jumatano inajumuisha kuitaka serikali ya Rais Donald Trump kuirudisha tena Korea Kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. 

Mwenyekiti wa kamati hiyo ndogo ya Bunge ya eneo la Asia na Pacific, Ted Yoho alitaja mfano wa mauaji ya Kim Jong Nam, kaka wa kambo wa kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa ndege nchini Malaysia hivi karibuni.

Alisema Kim aliuawa kwa kutumia kemikali ya sumu aina ya VX inayoathiri mishipa ya fahamu ambayo ni sawa na silaha ya maangamizi. Kamati hiyo pia imepitisha muswada au mapendekezo kuhusu kuiwekea vikwazo vikali Korea Kaskazini.

Muswada huo unairuhusu serikali ya Marekani kuchukua hatua za kuwaadhibu raia wa kigeni watakaonunua rasilimali za asili na bidhaa za kilimo kutoka Korea Kaskazini. Pia inapendekeza kuadhibu kampuni za kigeni zitakazoajiri raia wa Korea Kaskazini. 

Mapendekezo ya muswada huo yanaonekana kuilenga China ambayo inafanya mihamala mingi na Korea Kaskazini. Eliot Engel, mbunge wa Bunge la Congress la Marekani ambaye ni mmoja wa watu waliounga mkono muswada huo alisema China pekee ndiyo yenye ushawishi kwa Korea Kaskazini, kwa hiyo inatakiwa itoe ushirikiano zaidi ili kutekeleza hatua hizo.
Kamati ya Bunge la Marekani lapitisha hatua kali dhidi ya Korea Kaskazini Kamati ya Bunge la Marekani lapitisha hatua kali dhidi ya Korea Kaskazini Reviewed by Bill Bright Williams on 12:56:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.