Updated Thursday, March 9, 2017

CIA na M15 wanatumia Samsung TV kwa upelelezi, hata kama TV imezimwa


Shirika la kijasusi la Marekani CIA na M15 wana uwezo wa kuingilia na kusikia kila kitu kinachoongelewa na watazamaji wa TV za Samsung hata kama TV hizo zitakuwa zimezimwa, WikiLeaks wameligundua hilo, na sasa yamebaki maswali mengi yasiyo na majibu kwa wale wote wanaotumia TV hizi duniani kote.

Mwaka 2014, CIA na M15 kwa ushirikiano waliweza ku-hack na kusikiliza kila kitu kilichokuwa kinaongelewa na watazamaji wa TV hizi, njia hiyo iliitwa "Weeping Angel."

Mbinu yao waliyohitumia waliweza ku-hack kwenye TV zote za aina ya Samsung F8000.

Hizi TV zote za F8000 series zina uwezo wa kuongozwa na watumiaji kwa kutumia sauti na (motion sensor) na zimeshasambazwa duniani kote.

TV za Samsung zinaongoza kwa mauzo duniani kote kwa miongo kadhaa sasa, zikiwa na share ya asilimia 21 mwaka 2015. Idadi ya TV za F8000 zilizouzwa duniani kote haijulikani.
CIA na M15 wanatumia Samsung TV kwa upelelezi, hata kama TV imezimwa CIA na M15 wanatumia Samsung TV kwa upelelezi, hata kama TV imezimwa Reviewed by Bill Bright Williams on 12:05:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.