Updated Monday, March 20, 2017

Chakula chenye sumu:Usinunue huyu samaki! Ataharibu afya yako na kukupotezea uhai


Ndugu zangu, yatupasa kuwa makini kwa kila aina ya chakula tunacho nunua! Kwanini? Hii ni kutokana kuna vyakula vingine kwa kiasi kikubwa vinapatikana kwenye supermarket, vyakula hivyo vinaweza kukuletea matatizo makubwa ya kiafya(GMO foods).

Wataalamu wanashauri usile huyu samaki, kwa sababu ni hatari sana kwa afya zetu! samaki huyu anajulikana kwa jina la Basa. Basa anauzwa kwenye mfumo wa barafu. Samaki huyu anapatikana sana mto Mekong huko nchini Vietnam, moja ya mito maarufu sana duniani. Samaki huyu anavuliwa kwenye visima ambavyo vina viwango vya juu vya sumu na bacteria.

Wataalamu wanaonya kuwa nyama ya samaki huyu inasindikwa kwenye compounds zenye sumu, zikiwemo chlorate, isomers na hexachlorobenzene.

Nchi ya Marekani tayari imepiga marufuku uingizwaji wa samaki huyu nchini mwao, wakionya kuwa samaki huyu amejazwa homoni ambazo zinamfanya akue kwa haraka na aongeze kuzaliana.

Cha kushangaza, samaki huyu anapatikana kwa bei rahisi sana supermarket, kitu ambacho kinawavutia wanunuaji kununua samaki huyu. Samaki huyu hana kirutubisho chochote, japo ni mtamu sana ukimla.
Chakula chenye sumu:Usinunue huyu samaki! Ataharibu afya yako na kukupotezea uhai Chakula chenye sumu:Usinunue huyu samaki! Ataharibu afya yako na kukupotezea uhai Reviewed by Bill Bright Williams on 10:34:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.