Updated Wednesday, March 8, 2017

Boko Haram washambulia msafara wa jeshi la Nigeria na kuteka askari wa kike


Afisa mmoja wa jeshi amesema Magaidi wa kundi la Boko Haram wameshambulia kwa ghafla msafara wa magari yaliyokuwa yamewabeba wanajeshi kaskazini mashariki mwa Nigeria ambapo wamewaua wanajeshi saba na kumteka mwanajeshi mmoja wa kike.

 Shambulizi hilo la jana lilifanyika karibu na mji wa Mafa kwenye njia kuu iliyoko kilomita 50 mashariki mwa Maiduguri. Mji huo wa kaskazini mashariki ndio chimbuko la kundi la Boko Haram na ambako ndiko operesheni ya jeshi la Nigeria imejikita zaidi katika mapambano dhidi ya kundi hilo ambalo tayari limesababisha vifo vya zaidi ya watu 20,000 tangu lilipoanza uasi wake miaka saba iliyopita.

 Mmoja wa wafanyakazi wa mashirika ya haki za binadamu amesema alisikia mawasiliano ya jeshi yakithibitisha shambulizi hilo. Jeshi la Nigeria mwaka jana lilifanikiwa kuwaondosha wanamgambo wa Boko Haram katika miji kadhaa nchini humo pamoja na maeneo ambayo ni ngome yao kuu lakini bado kundi hilo limekuwa likiendeleza mashambulizi yake katika maeneo kadhaa.


Boko Haram washambulia msafara wa jeshi la Nigeria na kuteka askari wa kike Boko Haram washambulia msafara wa jeshi la Nigeria na kuteka askari wa kike Reviewed by Bill Bright Williams on 10:45:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.