Updated Sunday, March 12, 2017

Assad: Vikosi vya Marekani nchini Syria havitakiwi - "Ni wavamizi"


Rais wa Syria, Bashar al-Assad amevilaani vikosi vya Marekani vilivyoingia nchini mwake, kwa kuviita kama vikosi vya uvamizi, vimekuja bila kualikwa.

"Vikosi vyovyote vinavyoingia nchini Syria bila mualiko au ruhusa, ni wavamizi tu, iwe ni Marekani, Uturuki au nchi nyingine yeyote ile,"Assad aliliambia shirika la habari la China.

Ingawa, Raisi wa Syria amesema kuwa ni uvamizi usiokubalika katika nchi yake, ila aliona ahadi ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya kuwa na dhamira ya kutaka kuwaangamiza Kabisa ISIS. Alisema, "tuna matumaini kwamba utawala wa Trump utaenda kutekeleza yale aliyosema"

Assad: Vikosi vya Marekani nchini Syria havitakiwi - "Ni wavamizi" Assad: Vikosi vya Marekani nchini Syria havitakiwi - "Ni wavamizi" Reviewed by Bill Bright Williams on 6:39:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.