Updated Friday, March 31, 2017

Aliyekuwa Raisi wa Korea Kusini Park Geun-hye amekamatwa


Waendesha mashitaka wa Korea Kusini wamemkamata aliyekuwa Raisi wa nchi hiyo Park Geun-hye baada ya mahakama kuidhinisha hati ya kukamatwa kwake. Mahakama kuu jijini Seoul ilimuhoji Park jana Alhamisi kwa muda wa saa nane.

Baada ya kuhojiwa, majaji wa mahakama waliamua kutoa hati ya kukamatwa kwake kabla ya alfariji ya leo Ijumaa. Waendesha mashitaka wamekuwa wakifuatilia makosa 13 ya jinai ambayo inasemakana aliyatekeleza.

Wakitafuta kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa Park, walisema makosa aliyotenda yalikuwa makubwa na kugusia kwamba kuna uwezekano wa Park kuharibu baadhi ya ushahidi.

Park ni raisi wa tatu aliyekuwa madarakani wa Korea Kusini kukamatwa. Baada ya kukamatwa, alipelekwa kwa gari la waendesha mashitaka hadi kizuizini takribani saa kumi alfajiri viungani mwa jiji la Seoul.Aliyekuwa Raisi wa Korea Kusini Park Geun-hye amekamatwa Aliyekuwa Raisi wa Korea Kusini Park Geun-hye amekamatwa Reviewed by Bill Bright Williams on 1:18:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.