Updated Thursday, February 9, 2017

Ufaransa ina Mipango ya kujenga Bullet Proof Glass karibu na mnara wa Eiffel


Manispaa ya Paris imetangaza mpango wake wa kujenga kioo chenye urefu wa mita 2.5 kwenda juu kuzunguka mnara wa Eiffel kama sehemu ya mpango utakao gharimu mamilioni ya fedha ili kusaidia kuzuia shambulio lolote la kigaidi litakalopangwa kufanyika katika eneo hilo ambalo ni maarufu sana kwa historia ya Ufaransa.

"Ugaidi bado ni tishio katika Paris na maeneo yote yenye kupendwa na watu wengi, ikiongozwa na mnara wa Eiffel,ni lazima zichukuliwe hatua maalum za kiusalama katika maeneo hayo" alisema Naibu Meya Jean-Francois Martins, ambaye anahusika na utalii katika  Paris City Hall.

Ukuta wa kioo ambao unakusudiwa kujengwa katika mnara wa eiffel ambao ulijengwa mnamo mwaka 1889, utazuia watu binafsi au hata magari yaliyotegwa mabomu kuharibu eneo hilo ambalo linatembelewa na watu zaidi ya milioni sita kwa mwaka.

Inasemekana ujenzi wa ukuta huo wa kioo utaanza mapema kipindi cha vuli ili kuchukua nafasi ya uzio wa fensi ya chuma uliokuwa umejengwa eneo hilo.
Ufaransa ina Mipango ya kujenga Bullet Proof Glass karibu na mnara wa Eiffel Ufaransa ina Mipango ya kujenga Bullet Proof Glass karibu na mnara wa Eiffel Reviewed by Bill Bright Williams on 3:34:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.