Updated Friday, February 17, 2017

Trump Kutoa amri mpya inayohusiana na Uhamiaji


Rais wa Marekani Donald Trump amesema wiki ijayo ataweka saini amri nyingine ya Raisi ya kuzuia wahamiaji. Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana Alhamisi, Trump kwa mara nyingine alizikosoa mahakama kuu zilizozuia amri yake ya muda inayopiga marufuku kusafiri ambayo aliitoa mwezi uliopita. 

Alieleza kuwa huo ni uamuzi mbaya uliofanyika na mahakama mbovu. Aidha, Raisi huyo amesema kuwa wiki ijayo atatoa amri nyingine ya Raisi ambayo italinda nchi kwa upana zaidi.

Awali Trump alipendekeza kuwa hatua nyingine zitafanyika mapema wiki hii. Aidha, hakuelezea kwa nini hatua hizo zimecheleweshwa wala hakuweka wazi taarifa zozote za amri hiyo mpya ya Raisi.

Amri hiyo iliyotolewa na Trump mnamo mwezi uliopita inawazuia kwa muda raia wa mataifa 7 ambao wengi ni Waislam pamoja na wakimbizi wanaotaka kuingia Marekani. 

Hata hivyo, mahakama kuu ya Washington imezuia amri hiyo kutekelezwa ambapo uamuzi huo uliungwa mkono na mahakama ya rufaa wiki iliyopita. Wasiwasi unaongezeka kuwa amri hiyo mpya ya Raisi huenda ikasababisha hali ya wasiwasi nchini humo kwa mara nyingine.
Trump Kutoa amri mpya inayohusiana na Uhamiaji Trump Kutoa amri mpya inayohusiana na Uhamiaji Reviewed by Bill Bright Williams on 2:50:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.