Updated Sunday, February 12, 2017

Toa sumu kwenye figo zako,Ugonjwa wa kisukari, Pumu na cholesterol kwa kutumia maji ya Bamia!


Bamia inaweza kutumika kama mboga, ina wingi wa vitamins, madini na virutubisho vingine vingi ambavyo vina faida sana katika afya zetu, mojawapo ni kutibu ugonjwa wa kisukari na kuzuia ugojwa wa figo.

Hata kama ukitumia bamia ikiwa mbichi, au imechemsha, hata kama imekaangwa na kupikwa, bado inakuwa na wingi wa faida katika miili yetu.

Hapa ni jinsi ya kutengeneza juisi ya Bamia:

1. Kata kila upande wa bamia kwa kisu
2. Weka bamia zilizokatwa kila upande katika jagi na kisha weka    maji ya kutosha.
3. Acha mchanganyiko huu wa bamia na maji angalau kwa masaa 8 au hata hadi masaa 24
4. Asubuhi didimiza maganda yote ya bamia chini ya jagi ili kuondoa virutubisho vyote    vilivyobaki kwenye maganda.
5.Toa maganda yote ya bamia kwenye maji na kisha kunywa hayo maji.

Faida nyingine za bamia kwa afya zetu ni pamoja na:

Bamia ina utajiri wingi wa fibre, vitamini muhimu na madini na ina nguvu ya kuchuja sumu, mboga hii ina faida sana kwa miili yetu kwa kuwa;
–  Kupunguza cholesterol
–  kuzuia kuvimbiwa
–  Kupunguza hatari ya aina fulani ya kansa, hasa colorectal cancer
–  Kuboresha viwango vya nishati na kuboresha dalili za uchovu
–  Kusaidia kutibu koo, irritable bowel,vidonda na uvimbe kwenye mapafu
Toa sumu kwenye figo zako,Ugonjwa wa kisukari, Pumu na cholesterol kwa kutumia maji ya Bamia! Toa sumu kwenye figo zako,Ugonjwa wa kisukari, Pumu na cholesterol kwa kutumia maji ya Bamia! Reviewed by Bill Bright Williams on 12:54:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.