Updated Wednesday, February 22, 2017

Rais wa Azerbaijan amteua mkewe kuwa makamu wakeRais Ilham Aliyev wa Azerbaijan amemteua mkewe Mehriban Aliyeva kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo.

Ofisi ya rais ilitangaza juzi Jumanne kuwa Mehriban Aliyeva ambaye ni mbunge ameteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Wadhifa huo ulianzishwa kufuatia kura ya maoni mwezi Septemba mwaka jana juu ya iwapo nchi hiyo ipanue mamlaka ya rais. Kwa sasa rais anaweza kumteua Makamu wa Kwanza wa Rais bila ya kuidhinishwa na bunge.
Rais wa Azerbaijan amteua mkewe kuwa makamu wake Rais wa Azerbaijan amteua mkewe kuwa makamu wake Reviewed by Bill Bright Williams on 5:39:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.