Updated Saturday, February 18, 2017

Raia wa Korea Kaskazini achunguzwa kuhusiana na kifo cha Kim Jong Nam


Polisi nchini Malaysia inachunguza endapo mwanaume mmoja raia wa Korea Kaskazini anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Kim Jong Nam alikuwa na mawasiliano yoyote na maafisa wa kijasusi wa nchi yake ya Korea Kaskazini. Kim Jong Nam ni kaka wa kambo wa Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Juzi Ijumaa polisi nchini Malaysia ilimshikilia Ri Jong Chola mwenye umri wa miaka 46 kwenye nyumba yake iliyoko kwenye viunga vya jiji la Kuala Lumpur. Majirani wamesema Ri alihamia kwenye nyumba hiyo akiwa na familia yake takribani mwaka mmoja uliopita. 

Jana Jumamosi maafisa wa polisi walimchukua mtuhumiwa huyo na kumpeleka kituo cha polisi kilichoko karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur. 

Jumatatu iliyopita Kim Jong Nam alianza kuumwa alipokuwa uwanja wa ndege na akafariki alipokuwa njiani akipelekwa hospitali. Maafisa wa idara ya Ujasusi ya Korea Kusini wamesema majasusi wa Korea Kaskazini walimwekea Kim sumu iliyosababisha kifo chake.

Vyombo vya habari vya Malaysia vimesema Ri ni mmoja kati ya wanaume wanne ambao inaaminika waliwaagiza wanawake wawili kumwekea sumu Kim. Wanawake hao mmoja akiwa raia wa Indonesia na mwingine akiwa na hati ya kusafiria ya Vietnam kwa sasa wako chini ya ulinzi wa polisi. Vyombo vya habari vinasema polisi wanaendelea na msako wa watu wengine watatu.
Raia wa Korea Kaskazini achunguzwa kuhusiana na kifo cha Kim Jong Nam Raia wa Korea Kaskazini achunguzwa kuhusiana na kifo cha Kim Jong Nam Reviewed by Bill Bright Williams on 10:57:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.