Updated Tuesday, February 14, 2017

China wazindua karatasi Sugu kwa Moto na Maji


Wanasayansi wa Kichina wamezindua karatasi kwa mara ya pili tena.

Karatasi hizi tunazozitumia kwa sasa zilizinduliwa nchini China mnamo karibu ya miaka 2,000 iliyopita....

Kwa awamu hii tena China wamezindua karatasi ambayo hailowi (water proof) na haichomeki (fire-resistant).

Wanasayansi hawa wa China wametengeneza karatasi ambayo ina uwezo mkubwa wa kuzuia maji na inaweza kuhimili joto la hadi 200 celsius.

Nadhani hii inahitajika zaidi kuzuia nyaraka muhimu kutopata ajali na kuharibika.

Timu ya utafiti kutoka Shanghai Institute of Ceramics ikiongoza na Professor Zhu Yingjie wametengeneza aina pekee ya karatasi duniani ambayo inaweza kuzuia maji yasipenye na pia kuzuia moto.

Wanasayansi hawa wameongezea aina fulani ya calcium ijulikanayo kama hydroxyapatite, inayopatikana katika meno ya wanyama na mifupa.

Karatasi hii ina muonekano sawa na karatasi ya kawaida, sema tu ina ulaini kidogo katika uso wake. Watafiti wanasema karatasi hii ina uwezo wa kuzuia kahawa, juice au chai ikimwagikia kwenye hii karatasi na pia ina uwezo mkubwa wa kuzuia joto hadi nyuzi 200 celsius.
Na pia karatasi hii inaweza kufutwa vizuri na maji bila ya hata kuharibu kilichoandikwa kwenye hiyo karatasi.

Karatasi hizi zitaanza kuwa sokoni rasmi baada ya miaka mitatu.

January 2015, moto nchini Urusi uliharibu mamilioni ya karatasi za kihistoria katika maktaba ya chuo kikuu cha INION RAN, tukio ambalo baadhi ya vyombo vya habari vilieleza kama  “cultural Chernobyl”.

Tunashukuru kwa karatasi hizi mpya, nyaraka muhimu za kizazi na kizazi zitabaki kuwa salama.
China wazindua karatasi Sugu kwa Moto na Maji China wazindua karatasi Sugu kwa Moto na Maji Reviewed by Bill Bright Williams on 10:59:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.