Updated Tuesday, October 11, 2016

Uzalishaji wa Samsung Galaxy Note 7 wasitishwa kwa milipuko ya betri


Kampuni kubwa ya teknolojia ya Samsung imetangaza kusitisha uzalishaji wa simu zake mpya aina ya Galaxy Note 7 kwa muda kutokana na kesi za ulipukaji wa betri.

Kampuni hiyo imeharifu kuchukuwa uamuzi huo kutokana na kesi zilizoongezeka kuhusu ulipukaji wa betri zake licha ya kufanyiwa ukarabati.

Afisa mmoja mkuu wa kitengo cha uzalishaji wa simu za Samsung alitoa maelezo na kutangaza kusimamishwa kwa shughuli ya utengezaji wa Galaxy Note 7 kwa ajili ya kujali usalama wa wateja wao kote ulimwenguni.

Kulingana na ripoti iliyotolewa, kesi nane za malalamiko ya betri ziliwahi kuwasilishwa kutoka kwa wateja wa Marekani, Korea Kusini, China na Taiwan.

Hatua hiyo imeweza kuchukuliwa ili kuepuka hali ya kuchafuliwa jina kampuni ya Samsung hadi itakapoweza kutatua tatizo hilo.

Samsung inakadiriwa kupoteza kiwango kikubwa cha faida baada ya kutoa tangazo la kurudishwa kwa simu za Galaxy Note 7 punde tu baada ya matatizo ya milipuko ya betri kuanza.

Uzalishaji wa Samsung Galaxy Note 7 wasitishwa kwa milipuko ya betri Uzalishaji wa Samsung Galaxy Note 7 wasitishwa kwa milipuko ya betri Reviewed by Bill Bright Williams on 12:01:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.