Updated Wednesday, October 12, 2016

Putin amewaambia Warusi wote waliopo nje za nchi:'Rudini Nyumbani Upesi'


Vladimir Putin ameagiza familia zote za Urusi na watoto wao wanaosoma nje ya nchi kurudi nyumbani mara moja, baada ya hofu kuongezeka juu ya uwezekano wa kutokea vita kuu ya tatu ya dunia.

Watoto wote inawapasa kurudi Urusi haraka kwa usalama wao wenyewe, kwa mujibu wa ripoti iliotolewa jana jumanne na Putin katika vyombo vya habari.

Vyanzo vya kiitelijensia nchini Urusi vinaamini kwamba vita kuu na Marekani ipo mbioni zaidi kutokea kuliko ilivyokuwa inakusudiwa miongo kadhaa iliyopita.Serikali na vyombo vya habari nchini humo vimeonya watu kujiandaa kwa ajili ya shambulio la nyuklia, baada ya Marekani kutangaza "kukata mahusiano" na Urusi kuhusu vita vya Syria.

Jeshi na wataalam wa mikakati wameonya kwamba mgogoro wa Syria sio kwamba ni vita vya wenyewe kwa wenyewe kama Marekani inavyosema.Vita vya Syria ni kichocheo halisi cha mlipuko wa vita kuu inayosubiri kulipuka.

Nchi zote zenye nguvu duniani sasa zimeelekea Syria. Pamoja na mvutano wa juu uliopo nchini Syria, Rais wa Urusi ana nia thabiti ya kuwalinda watu wake kwa gharama zozote zile.

Wiki iliyopita Vladimir Putin aliamuru kila mji nchini Urusi kushiriki katika mazoezi ya dharura, yasiyokuwa ya kawaida kwa ajili ya ulinzi wa raia, dharura hiyo ilidumu siku nne-na watu zaidi ya milioni 40 karibu theluthi moja ya nchi- walishiriki katika mazoezi hayo ya kujihami endapo shambulio la nyuklia litatokea nchini humo.

Tangazo kutoka kwa mawaziri wa Putin zinasema kwamba serikali imejenga nyuklia bankers zenye uwezo wa kuhifadhi watu milioni 12 wa mji wa Moscow, katika tukio la shambulio lolote litakaloweza kutokea katika mji huo.Picha hapo juu ni moja ya nyuklia banker endapo shambulio lolote la nyuklia likitokea nchini humo basi watu watakao ingia humo ndani watanusurika, hawatadhurika.


Putin amewaambia Warusi wote waliopo nje za nchi:'Rudini Nyumbani Upesi' Putin amewaambia Warusi wote waliopo nje za nchi:'Rudini Nyumbani Upesi' Reviewed by Bill Bright Williams on 6:16:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.