Updated Friday, October 7, 2016

Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Marekani


Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini jana Alhamisi iligusia uwezekano wa nchi hiyo kufanya kitendo cha kichokozi ikisema kuwa Marekani itakabiliana na ukweli wa kuogofya katika siku zijazo. 

Onyo hilo limekuja kabla ya siku ya kusherehekea kuanzishwa kwa chama tawala cha nchi hiyo, Oktoba 10. Marekani imekuwa ikiongeza shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini kutokana na uendelezaji wa nyuklia na makombora unaofanywa na nchi hiyo.

Katika taarifa moja, msemaji wa Korea Kaskazini alilitaja jina la Rais wa Marekani bila ya kuutambulisha wadhifa wake. Alisema kuwa sera za chuki za Marekani na shinikizo lao wakitumia vitisho vya nyuklia na jeshi vimesababishia Korea Kaskazini kuwa kile nchi hiyo inaita nchi yenye nguvu kubwa ya nyuklia.

Taarifa hiyo pia imeikosoa Marekani kwa kutoa wito kwa nchi zingine kuvunja mahusiano na Korea Kaskazini na ikaashiria madhara yatokanayo na sera kama hizo.

Shirika la habari linalomilikiwa na Korea Kaskazini mwezi uliopita lilisema kuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un aliamuru maandalizi yasiyopingika ya urushaji wa kombora la masafa marefu. Kombora lingine kama hilo lilirushwa mwezi Februari.
Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Marekani Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Marekani Reviewed by Bill Bright Williams on 3:36:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.