Updated Friday, August 12, 2016

Wanasayansi wavumbua njia salama ya kupanga uzazi kwa wanaume


Wanasayansi wamefanikiwa kubaini njia ya kutumia mafuta kupanga uzazi kwa wanaume ambayo itawezekana kuruhusu mwanaume kuzaa baada ya muda, matokeo ambayo yamefanikiwa vizuri kwa wanyama, na huenda mafuta hayo yakaanza kupatikana katika kipindi cha miaka miwili au mitano ijayo.

Kugunduliwa kwa mafuta haya huenda kukabadili uelekeo wa njia za kupanga uzazi, huku wanaume wakitarajiwa kuhusishwa moja kwa moja kwenye uzazi wa mpango katika familia.

Wanasayansi wanasema kuwa, kuhusishwa kwa wanaume kwenye uzazi wa mpango ndani ya familia, kutasadia pia kuzuia mimba.

Mafuta haya "vasalgel" yanatarajiwa kuwa njia mbadala kwa wanaume kuzuia mimba sambamba na matumizi ya mpira wa kiume na kuepuka ngono.

Mafuta haya ambayo yatakuwa kwenye mfumo wa majimaji, yatachomwa kama sindano kwenye mirija inayopitisha manii kutoka kwenye korodani, ambapo yatatengeneza kinga itakayozifanya mbegu za mwanaume zisiwe na uwezo wa kuzalisha na kuzizuia kupita.


Mafuta haya yatachomwa kwenye mirija yote miwili ya mwanaume.

Wanasayansi wanasema kuwa njia hii itaweza kukaa hadi kufikia miaka 10, na kuongeza kuwa athari zake huenda zisionekana mapema kwakuwa kuna baadhi ya manii yatakuwa yanabaki kwenye mirija.

Mafuta haya yatakuwa na uwezo wa kuzuia kuzaliwa kwa manii mpya.

Ikiwa mwanaume atataka kurejesha mzunguko wa kawaida wa mbegu za kiume, iwe kwa mwaka mmoja au hata mwezi, sindano maalumu itapitishwa kwenye mirija kuyeyusha mafuta ya awali kuruhusu uzalishaji wa kawaida kuendelea.
Wanasayansi wavumbua njia salama ya kupanga uzazi kwa wanaume Wanasayansi wavumbua njia salama ya kupanga uzazi kwa wanaume Reviewed by Bill Bright Williams on 12:32:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.