Updated Sunday, August 7, 2016

Somalia kufanya uchaguzi wa rais mwezi Oktoba mwaka huu


Tume ya uchaguzi ya Somalia imetoa ratiba ya mchakato wa uchaguzi ujao ambao utakamilika kwa kumchagua rais mpya wa nchi hiyo tarehe 30 Oktoba.

Mwenyekiti wa tume hiyo Omar Mohamed Abdulle amesema, uchaguzi wa baraza la bunge na uchaguzi wa wabunge utafanyika Septemba na Spika wa bunge atachaguliwa Oktoba. Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa serikali, mikoa, na jumuiya za kimataifa kutoa ushirikiano katika kukamilisha mchakato wa uchaguzi na kutoa msaada unaotakiwa kwa upande wa usalama na vifaa vya uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa mafanikio.

Serikali, bunge, na mahakama pamoja na viongozi wa mikoa nchini Somalia wamekubaliana kuwa muda wa serikali iliyoko madarakani sasa hautaongezwa tena pale utakapomalizika mwezi ujao.
Somalia kufanya uchaguzi wa rais mwezi Oktoba mwaka huu Somalia kufanya uchaguzi wa rais mwezi Oktoba mwaka huu Reviewed by Bill Bright Williams on 11:29:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.