Updated Monday, August 1, 2016

Msomi wa Marekani asema mfumo wa Makombora(THAAD) kuwekwa Korea Kusini ni uamuzi wenye makosa


Mkuu wa idara inayopitia taarifa za kijasusi ya kimataifa ya Marekani huko Washington Bw. William C Jones amesema mfumo wa kuzuia makombora wa THAAD kuwekwa nchini Korea Kusini ni uamuzi wenye makosa, na utatishia amani na utulivu wa Asia.

Bw Jones amesema, Korea Kusini kukubali kuwekwa kwa mfumo huo nchini humo kunafuatia majaribio ya nyuklia yaliyofanywa hivi karibuni na Korea Kaskazini na pia kutokana na shinikizo la Marekani. Lakini kwa mujibu wa watafiti, mfumo huo hauwezi kuzuia makombora kutoka Korea Kaskazini, na badala yake utaichochea Korea Kaskazini.


Ameongeza kuwa mbali na kuathiri maslahi ya China na Russia, Marekani nayo pia haitanufaika na kitendo hicho, ambacho kitavunja amani na utulivu wa Peninsula ya Korea na eneo la Pacific.
Msomi wa Marekani asema mfumo wa Makombora(THAAD) kuwekwa Korea Kusini ni uamuzi wenye makosa Msomi wa Marekani asema mfumo wa Makombora(THAAD) kuwekwa Korea Kusini ni uamuzi wenye makosa Reviewed by Bill Bright Williams on 12:57:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.