Updated Sunday, August 7, 2016

Donald Trump awageukia wakimbizi toka Somalia


Mgombea urais kupitia chama cha Republican, Donald Trump ameongea kwa hasira kwa kuwashutumu miongoni mwa wakimbizi wa Somalia nchini Marekani, kwa kuwalaumu wao kwa ongezeko la uhalifu na waislam wenye msimamo mkali nchini humo.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Portland city of Maine, Trump alipendekeza kuwa utitiri wa wakimbizi wa Somalia ni hatari kwa usalama wa jiji hilo. Amewalaumu wakimbizi hao kwa ongezeko la uhalifu katika eneo hilo.

Jamii ya Wasomali wa Portland wamelaani vikali maneno ya Trump. Wao wanamuelezea mgombea huyo uraisi kwa tiketi ya Republican kuwa ni muharibifu na anaharibu tamaduni za jamii yao.

Trump anatetea maneno yake na anapinga uhamiaji wa wakimbizi kutoka Somalia.

Donald Trump awageukia wakimbizi toka Somalia Donald Trump awageukia wakimbizi toka Somalia Reviewed by Bill Bright Williams on 1:48:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.