Updated Saturday, August 6, 2016

Chama cha ANC chashindwa vibaya uchaguzi wa serikali za mitaa


Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimepata pigo kubwa baada ya kushindwa vibaya kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo chama cha Alliance Democratic DA kimeshinda , tume ya uchaguzi imetangaza jana Jumamosi.


Akizungumzia matokeo hayo mabaya ya uchaguzi kwa chama hicho tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu wachache miaka 22 iliyopita, Rais Jacob Zuma amesema kuwa wapiga kura wamesikika.

Rais Zuma ambaye anakabiliwa na maswali kuhusu nafasi yake baada ya uchaguzi,amesema "Uchaguzi huo ulikuwa na mpambano mkali, na ndivyo inavyopaswa kuwa katika demokrasia.

Huko Tshwane, eneo la mji mkuu linalojumuisha mji wa Pretoria, chama cha DA kimeshinda kwa asilimia 43 ya kura huku chama cha ANC kikipata asilimia 41, kwa mujibu wa matokeo ya mwisho katika uchaguzi ambao umedhihirisha kupungua kwa umaarufu wa chama hicho ambacho kiliongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Kushindwa huku kwa chama cha ANC kunakuja baada ya chama hicho kushindwa katika mji wa Port Elizabeth hapo jana, katika mpambano mkali wa uchaguzi wa serikali za mitaa.


Chama cha ANC chashindwa vibaya uchaguzi wa serikali za mitaa Chama cha ANC chashindwa vibaya uchaguzi wa serikali za mitaa Reviewed by Bill Bright Williams on 11:42:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.