Updated Thursday, July 21, 2016

Wakulima watishia kuwaua Tembo kwa sumu nchini Kenya


Wakulima nchini Kenya wa kaunti ya Laikipia wametishia kuwaua ndovu wa eneo hilo kwa sumu kwa sababu wanavamia sana mashamba yao. 
Wanasema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya serikali kushindwa kuwazuia wanyama hao kuvamia mashamba yao. Wakulima hao wamesema mimea yao imekuwa ikiharibiwa na wanyama hao na licha ya kutoa ripoti kwa maofisa wa shirika la wanyama pori KWS hakuna hatua ambayo imechukuliwa ya kuwazuia ndovu hao. 
Wakati huo huo Maofisa wa serikali kuu katika eneo la Ganze wameomba usaidizi zaidi wa chakula kupelekwa katika eneo hilo. Maofisa hao wamesema zaidi ya watu laki 1 wanakabiliwa na njaa kutokana na ukame wa muda mrefu ambao umekausha kabisa mimea katika sehemu hiyo.
Inadaiwa chakula cha tani 10 ambacho kilitolewa na serikali kimekuwa kidogo na hakiwezi kutosheleza kila mtu. Waathiriwa wakubwa wa baa hilo la njaa ni watoto wa shule, walemavu, wajane na wakongwe ambao hali zao za kiafya zimekuwa kikwazo kikuu cha kupata chakula.
Wakulima watishia kuwaua Tembo kwa sumu nchini Kenya Wakulima watishia kuwaua Tembo kwa sumu nchini Kenya Reviewed by Bill Bright Williams on 5:52:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.