Updated Sunday, July 24, 2016

Urusi imesema: Marekani inawasaidia magaidi wanaoua watoto wa Palestina


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa, ripoti zinaonesha kuwa, watu waliomchinja mtoto wa Kipalestina na kuonesha mkanda wa video wa kitendo cha kukata kichwa cha mtoto huyo katika mitandao ya kijamii wanasaidiwa na kuungwa mkono na Marekani.

Maria Zakharova amesema kuwa, magaidi hao wanaotajwa na baadhi ya nchi kuwa ni wapinzani wenye misimao ya wastani, walimuua kikatili mtoto huyo wa Palestina kwa madai kwamba alikuwa miongoni mwa waungaji mkono wa Rais Bashar Asad wa Syria. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameongeza kuwa, mtoto huyo aliyeuawa kikatili alikamatwa karibu na mji wa Halab (Aleppo) na alama zinazoonekana juu ya mwili wake zinaonesha kuwa alipewa mateso kabla ya kuuliwa.

Zakharova amesisitiza kuwa, makundi hayo yanayoungwa mkoni na Marekani ni ya kigaidi na wala hayana chembe ya thamani na maadili ya kibinadamu.

Jumanne iliyopita kundi la kigaidi lilalojiita Nureddin al-Zenki lilitenda ukatili wa kutisha wa kumchinja mtoto Abdullah Issa wa Kipalestina aliyekuwa akiishi katika kambi ya wakimbizi ya Handarat huko Halab wakilipiza kisasi dhidi ya harakati za mapambano za Palestina.  
Urusi imesema: Marekani inawasaidia magaidi wanaoua watoto wa Palestina Urusi imesema: Marekani inawasaidia magaidi wanaoua watoto wa Palestina Reviewed by Bill Bright Williams on 5:27:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.