Updated Thursday, July 21, 2016

Unasumbuliwa na Kisukari, chemsha majani haya na tatua tatizo lako


Kisukari kimeathiri afya za watu wa rika mbalimbali duniani kote, na watu wengi wanasumbuliwa na aina mojawapo ya kisukari. Hii inatokana na upungufu wa insulin zinazozalishwa na kongosho au mwili kukosa uwezo wa kutumia vizuri insulin hiyo.

Hizi ni dalili za kawaida  za Kisukari
-Kuwashwa sehemu za siri
-Jeraha ambalo linachelewa sana kupona
-Kiwewe
-Kujisikia kuchoka sana
-Kukojoa mara nyingi zaidi kuliko kawaida, hasa wakati wa usiku
-Kuhisi kiu sana
-Uzito kupungua ghafla
-Kisukari pia kinaweza sababisha kutoona vizuri,upofu, udhaifu, maradhi ya moyo na figo kushindwa kufanya kazi.

Aina za Kisukari

Kisukari 1, pia kinajulikana kama juvenile diabetes, kinatokea pale ambapo mfumo wa kinga kimakosa unashambulia na kuharibu beta seli za kongosho ambayo inazalisha insulin.

Kisukari 2, pia kinafahamika kama kisukari cha watu wazima, inatokea pale mwili kukosa uwezo wa kutumia insulin au kuwa na upungufu wa uzalishwaji wa insulin.

Gestational diabetes, huathiri wanawake wajawazito, hasa semister ya pili ya mimba.

Pengine umeshawai kusikia tiba nyingi za asili zinazoweza saidia kuweka vizuri viwango vya sukari katika damu, lakini tiba niliyotoa katika makala hii ni nzuri na madhubuti. Tiba hii inahusisha majani ya maembe, ambayo wengi wanajua faida za majani haya kwa afya.

Majani ya maembe yana wingi wa vitamini, madini, Enzymes na antioxidants.Yana uwezo wa kutibu masuala mbalimbali katika afya ya binadamu, kama vile kuhara, kukosa usingizi, pumu,
homa,  bronchitis, na varicose veins. Aidha yana uwezo wa kuimarisha mishipa ya damu na kushusha shinikizo la damu.

Kichocheo

Maelekezo:
-Chukua majani 10-15 ya maembe na yachemshe kisha yaweke kwenye glasi
-Yaache yakae usiku kucha
-Yachuje ifikapo asubuhi na kunywa hayo maji ukiwa tumbo tupu
- Kwa matokeo mazuri, tumia kinywaji hiki kwa mda wa miezi 2-3

Njia nyingine unayoweza kutumia haya majani ya maembe, ni kuyakausha na kuyaponda.
Tumia nusu kijiko cha haya majani mara mbili kwa siku.
Unasumbuliwa na Kisukari, chemsha majani haya na tatua tatizo lako Unasumbuliwa na Kisukari, chemsha majani haya na tatua tatizo lako Reviewed by Bill Bright Williams on 6:49:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.