Updated Wednesday, July 20, 2016

Trump ateuliwa rasmi kuwa mgombea kiti cha rais wa republican


Wajumbe wa chama cha republican wamepiga kura kumteua mgombea wao rasmi July 19, 2016.

Tajiri wa majumba Donald Trump ameteuliwa rasmi kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Republican katika uchaguzi ulofanyika katika mkutano mkuu wa chama hicho mjini Cleveland, Ohio .

Katika utaratibu wa wajumbe wa kila jimbo kujitokeza na kutangaza kura zao wanampa nani, Trump alipata kura 1347 zinazohitajika kuwa mgombea wa chama hicho.


Uwamuzi huu umetokea baada ya kuwepo na shaka kwamba huwenda wajumbe wa chama hicho wakagawika na kutompa mwanabishara huyo anaegeuka kua mwanasiasa kura zao.

Huu ni uwamuzi wa kihistoria kwa chama hicho kutokana na kumteua mtu asie mwanasiasa na ambae hakua mwanachama wa dhati wa chama hicho.

Baadhi ya viongozi wa chama wamesusia mkutano huu na kulikua na wasiwasi kutakuwepo na mvutano hadi mwisho wa mkutano hasa baada ya kundi la kumpinga Trump lilipojaribu kuzuia utaratibu wa kanuni kuendelea.
Trump ateuliwa rasmi kuwa mgombea kiti cha rais wa republican Trump ateuliwa rasmi kuwa mgombea kiti cha rais wa republican Reviewed by Bill Bright Williams on 1:32:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.