Updated Saturday, July 2, 2016

Shambulizi la kigaidi latekelezwa katika mkahawa wa chakula Bangladesh


Watu wawili wafariki, 20 watekwa nyara kwenye shambulizi la kigaidi lililotekelezwa katika mgahawa mmoja wa chakula nchini Bangladesh. Maafisa wawili wa polisi wameripotiwa kupoteza maisha kwenye shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na kundi la ISIS katika mgahawa mmoja wa chakula nchini Bangladesh.
Watu wengine 20 wakiwemo raia kadhaa wa kigeni pia wameripotiwa kuchukuliwa mateka na magaidi baada ya shambulizi hilo lililotekelezwa katika eneo la Gulshan lililoko mjini Dakka.

Kikosi cha usalama kiliwasili kwenye tukio na kufanikiwa kuwaangamiza magaidi 6 ambao ni miongoni mwa walioshambulia eneo hilo lenye majengo ya balozi za nchi mbalimbali.

Takriban maafisa 100 wa kikosi cha usalama waliendesha operesheni ya kuwasaka magaidi waliowachukuwa mateka watu 20 na kufanikiwa kuwaokoa mateka hao.
Tangu mwaka 2013 hadi kufikia sasa, wafanyakazi zaidi ya 20 wa mashirika ya habari, viongozi wa kidini na mashirika ya umma wameripotiwa kuuawa kwenye mashambulizi yanayotekelezwa mara kwa mara.


 
Shambulizi la kigaidi latekelezwa katika mkahawa wa chakula Bangladesh Shambulizi la kigaidi latekelezwa katika mkahawa wa chakula Bangladesh Reviewed by Bill Bright Williams on 1:26:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.