Updated Tuesday, July 19, 2016

Rais Putin atuma salamu za rambi rambi kwa Uturuki


Rais Putin akemea jaribio la mapinduzi Uturuki na kufahamisha kukutana na rais Erdogan mwezi ujao

Rais wa Urusi Vladimir Putin atoa salamu za rambi rambi kwa Uturuki baada ya jaribio la mapinduzi lililosababisha  vifo vya watu zaidi ya 160 na kulaani vikali jaribio hilo.

Vladimir Putin alimpigia simu rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kumpa pole kwa niaba ya Urusi kufuatia jaribio la mapinduzi lililotekelezwa na kundi la wanajeshi walioasi.

Rais Putin amefahamisha kuwa anataraji kuona hali ya usalama na utulivu ikizidi kuhimarika nchini Uturuki.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamepanga kukutana katika wiki ya kwanza ya mwezi ujao.
Rais Putin atuma salamu za rambi rambi kwa Uturuki Rais Putin atuma salamu za rambi rambi kwa Uturuki Reviewed by Bill Bright Williams on 12:11:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.