Updated Thursday, July 28, 2016

Papa Francis aanguka nchini Poland


Katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa bahati mbaya, kiongozi wa kanisa KATOLIKI duniani, Papa Francis wa kwanza  mwenye umri wa miaka 79 alianguka chini, alipokuwa akiongoza misa nchini Poland, ya siku ya vijana duniani.

Video ikumuonyesha Papa Francis akianguka

Tukio hilo limetokea wakati Papa akibariki, waumini waliohudhuria misa hiyo, akiwa katika ziara yake ya siku tano nchini Poland.

Papa alisaidiwa na wasaidizi wake, na inaeonekana hakuumia katika tukio hilo.


Asilimia karibia 88%  ya raia wote wa Poland ni wakatoliki, na wamekuwa wakiendeleza imani yao, licha ya nchi hiyo kupitia katika kipindi cha siasa za kikomunisti.
Papa Francis aanguka nchini Poland Papa Francis aanguka nchini Poland Reviewed by Bill Bright Williams on 4:58:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.